Wednesday, November 5, 2014

KWELI MAJANGA: BINT ALIYEJIPATIA UMAARUFU MKUBWA KWA PICHA ZA UCHI KUGOMBEA UBUNGE 2015, TAYARI AMESHACHUKUA FOMU ZA CHAMA KIMOJA MAARUFU NA CHA SIKU NYINGI NCHINI..!

Na Sakina Shabani
Mmh hakika taifa letu lililojaliwa na Mungu kwa upendo na amani linakwenda kuangamia sasa kwa kupa viongozi wasio kuwa na maadili kufuatia msichana pichani aliyefahamika kwa jina la Cleopatra Mushi ambae aliwahi kutingisha mji kwa picha zake za uchi sasa anakwenda kuingia mjengoni kututetea wananchi.
Taarifa sahihi zilizonaswa na mtandao huu hatari kwa habari za uchunguzi wa maskanibongotz imebaini kuwa Cleopatra ambae wakati anasambaza picha zake hizi alikuwa akisomea Sheria chuo kimoja maarufu Mkoani Iringa na baadae akawa mwanasheria wa kujitegemea na sasa amejiingiza kwenye siasa kwa lengo moja la kuingia mjengoni 2015 kwa ajili ya kuwatetea wananchi wake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kisichokuwa na shaka hata kidogo kilisema" Jamani kweli nchi inaenda kuangamia huyu dada kuna taarifa amechukua fomu ya kujiunga na chama kimoja kikongwe cha Siasa anataka kugombea Ubunge kupitia jimbo moja huko Moshi sasa sijui wananchi watajifunza nini kupitia kwake" Aliema
Hata hivyo habari zaidi zilielezwa msichana huyo ambae anatoka familia yenye maadini ya maana na pia ni wamiliki wa kampuni ya mabasi ya kwenda mikoa ya Arusha Kilimanjaro Mwanza ameungwa mkono na familia yake huku wakijitahidi sana kuficha skendo ya picha ili wanasisa wasijue uchafu aliowahi kuufanya.
CREDIT: MASKANIBONGOTZ

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king