Thursday, October 23, 2014

MSANII MANAIKI SANGA AMFUNDA DIAMOND AMWAMBIA NI HERI AKAACHANA NA MUZIKI KWA SASA ILI ALINDE HESHIMA YAKE LA SIVYO HALI ITAZIDI KUWA MBAYA KWAKE..!

Msanii Manaiki Sanga akiwa na Wema Sepetu ambapo picha hii iliwahi kuzusha balaa kubwa nchini Tanzani kiasi cha kuhatarisha mahusiano ya Wema na Diamond
 

Na Mwandishi Wetu
Mwanamuziki na msanii wa bongo Movie Manaiki Sanga  The Don ametoa ushauri mzito kwa mwanamuziki Naseeb Abdul  a.k.a Diamond na kusema kuwa mwanamuziki huyo anatakiwa kusoma alama za nyakati kipindiu cha ufalme wake kimefika kikomo anatakiwa sasa hivi kuachana na muziki badala yake afanye biashara tu.
Akiongea na mtandao Bossngasa Manaiki Sanga alisema" Napenda kumshauri Diamaond kwa sasa angestaafu kuimba badala yake afanye biashara kwa vile tayari amejikusanyia visenti kidogo na hapo atalinda heshima yake aliyojijengea muda mrefu" Alisema
Hata hivyo msanii huyo aliongeza kusema kuwa kitendo cha kuanza kusomewa hadi Jijini Dar kitafungulia njia hata mikoani au nje ya nchi nako watamzomea au atarushiwa mawe hali itazidi kuwa mbaya zaidi ni heri akaachana na muziki kwa sasa na hii imewakuta wasanii wengi wa Tanzania akiwemo Mr Nice.


0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king