Wednesday, October 22, 2014

KUNDI LA MAKHIRIKHIRI LA BOTSWANA YAMTEUA MWANDISHI WA E-FM RADIO KUWA MSEMAJI WA KUNDI HILO..!




Na Mwandishi Maalum
Kundi la Makhirikhiri la nchini Botswana linaloangozwa na Moses Malapela a.k.a Shumba Latshega limemteua Bwa Livingstone Mkoi msemaji wa kundi hilo nchini Tanzania.
Akiongea na gazeti hili Livingstone Mkoi ambae ni mwandishi wa Habari wa kituo cha E-fm Radio Jijini Dar alisema “ Nilipigiwa simu na Shumba kiongozi wa kundi hilo  ambae ni rafiki yangu mkubwa na kunuieleza kuwa kuanzia sasa nitakuwa msemaji wa kundi hilo hapa nchini Tanzania ambako kundi hilo lina mashabiki wengi sana” Alisema Mkoi
Aidha katika taarifa hiyo Livingstone  aliongeza kusema tayari wameshaingia mkataba wa awali na kiongozi huyo na hivi karibuni mwanamuziki huyo atakuwepo nchini Tanzania kwa ajili ya kuja kuingia mkataba na kampuni LIBE PRODUCTION kwa ajili ya kusambaza albam yake mpya iitwayo  LASO LA MONAMOGOLO mbayo ni moto wa kuotea mbali.
Msemaji huyo aliongeza kusema kuwa katika albam hiyo ambayo baadhi ya nyimbo zake zimefanyiwa nchini Tanzania huku wakielezea usafiri wa bajaj ambao nchini Botswana haupo kabisa na wala hakuna kitu kinachoitwa bajaji.
Kundi la Makhirikhiri liliwahi kuja nchini 2010 na lililetwa na kituo cha Times Radio na kufanikiwa kukonga nyoyo za mshabiki na kuzunguka Tanzania nzima.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king