AUNT EZEKIEL AKIWA NA JACK PEMBA ENZI ZAO WAKATI WAKIWA MUME NA MKE
HAPA HATMAN AKIWA NA AUNT EZEKIEL WAKATI WAKI
MH. WAZIRI NYALANDU AKIWA NA MKEWE FARAJA KOTA
Na Mwandishi Maalum
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabishara
aliyekuwa mume wa msanii Aunt Ezekiel miaka ya nyuma Jack Pemba kabla ya
kumwagana ameibuka na kumtahadhalisha Mh Lazaro Nyalandu kuhusu msanii huyo na
kusema ni heri akasikia ushauri wake la sivyo yatamkuta makubwa.
Akiongea na mtandao wa mtandao huu Jack Pemba
alianza kusema “ Namsikitikia sana Mh Nyalandu kama kweli haya yanayozungumzwa
yana ukweli juu yake kama kweli ana mahusiano ya kimapenzi na Aunt Ezekiel na
anaupendo wa dhati na mkewe pamoja na familia yake basi ni heri akaachana nae
msanii huyo haraka kwani atakuja juta kuzaliwa” Alisema
Mfanya biashara huyo aliendelea kusemA “ Ant Ezekiel
ni mwanamke hatari sana sijawahi kuzungumza haya hata kidogo lakini leo hii
nawambia ukweli kama mwanamke huyo ni hatari sana ukishakuwa na mahusiano nae
ujue lazima ufirisike tu na mfano ni kwangu mimi kabla ya kuwa na Aunt nilikuwa
na pesa nyingi sana lakini nilivyokuwa nae basi pesa zote ziliyeyuka na
kunikimbia” Alisema mfanyabishara huyo
Aidha pedeshee huyo ambae aliwahi kumwaga kiloba cha
pesa kwenye ukumbi wa Bilicanas miaka ya nyuma wakati bendi ya Twanga Pepeta
ikitumbuiza na kusababisha fujo kubwa
aliendelea kusema “ Kwanza Aunt ni mwanamke anaejua sana mapenzi nadhani huenda
akawa namba moja Tanzania kwa wasichana hali hiyo humfanya mwanaume kushindwa
kumuacha hadi kupelekea kupururwa kila kitu” Alisema
Hata hivyo Jack alitolea mfano hata baada ya kuachwa
na Aunt alikimbia kwa Hatman Mbilinyi ambae ni kaka na Mbunge wa Jimbo la Mbeya
mjini Mh Joseph Mbilinyi ambae nae alifilimbwa kila kitu na kumuacha mtupu
kiasi cha kumpelekea kuanza upya maisha na familia yake.
Mfanyabishara huyo
alimaliza kusema kuwa kama hadi leo hii asingeachana na msanii huyo angekuwa
fukara wa kutupwa lakini kwa sasa amerejea utajiri wake wa zamani huku akaunti
zikiwa zimecheua mamilioni na muda mwingi siku hizi amekuwa akisaidia watoto
yatima.
0 comments:
Post a Comment