Haya ni mabomu ya kurushwa kwa mkono ambayo inadhaniwa huenda ndiyo yaliyotumika kulipua kituo cha polisi na kuua askari wetu.
Majambazi kama haya ni hatari sana na kama ikisindikana kuwahiwa wanaweza kuleta madhara makubwa kama haya ya Bukombe.
Pamoja na idadi ya matukio mengi ya Majambazi Tanzania imekua ni nadra
sana kusikia Majambazi wamevamia kituo cha Polisi na kusababisha mauaji
ya askari pamoja na kuiba silaha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana mkoa mpya wa Geita katika kituo cha Polisi Bukombe ambapo Majambazi hawa walivamia na kuwauwa askari polisi wawili na wengine wawili kujeruhiwa na kisha kuiba silaha kadhaa kutoka kwenye kituo hicho.
Majambazi wameingia kwenye rekodi za matukio makubwa 2014 baada ya wengine wanaoaminika kuwa raia wa Burundi, kuirushia daladala bomu la kutupa kwa mkono huko Kigoma baada ya daladala hiyo kugoma kusimama iliposhtukia mchezo wa kutaka kutekwa hivi karibuni.
CREDIT: MASKANIBOMNGOTZ.BLOGSPOT.COM
0 comments:
Post a Comment