Abdulrahman Kinana
Nape Nnauye
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kitongoji cha Nakasangwe mtaa wa madale kata ya Wazo ambao ni wanachama wa CCM wametishia kukihama chama hicho endapo uongozi wa CCM Kitaifa hawatawafika kwenye eneo hilo lenye mgogoro wa Ardhi kati ya mwenyezaji na wao.
Wakiongea na waandishi wa habari kituo cha E-FM RADIO hivi karibuni wananchi hao walisema kuwa CCM imewatelekeza bila msaada wowote licha kuwa na taarifa juu ya unyanyasaji wanaofanyiwa na viongozi wa Serikali wa Mkoa wanaodai kuwa anashirikiana na wawekezaji kuwapora ardhi yao.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha Mama Jasmin alisema" Sisi tunaishi maisha magumu sana awali walikuja na kutuambia sisi si watanzania lakini uchaguzi uliopita tulipiga kura na baada ya hapo tena wakaja kutuvunjia nyumba zetu wakidai tumevamia eneo hilo lakini ukweli hii si haki hata kidogo tunawaomba viongozi wetu wa CCM Nape Nnauye na Abdulrahman Kinana waje kutusikiliza pamoja na kutusaidia la sivyo hakika tuko tayari kuhama chama" Alisema mama huyo
Kata hivyo imekuwa ngome ya CCM miaka mingi huku upinzani ukiwa hauna nguvu ambapo hata uchaguzi wa 2010 CCM ilijinyakulia kura nyingi, na ndio maana wananchi wa huko wahawajawah kumfuata mbunge wao Halima Mdee na kumlalamikia matatizo yao.
0 comments:
Post a Comment