Friday, April 18, 2014

WATAMBUE WABONGO 10 WALIOPATA UMAARUFU KUPITIA MIGONDO YA WENZAO DIAMOND WA KWANZA. ANGALIA LIST HII UTAMUE UKWELI WA MAMBO!

Blog hii imeamua ikuletee list ya watu 10 ambao now days wamekuwa maarufu kupitilizalakini umaarufu wao wote umetokana na mtu fulani inamaana bila fulani wasingekuwa maarufu na kuzungumzwa katika jamii tuliyopo. tuanze countdown yetu kwa kuanzia namba 1 hadi namba 10

1. Agnes Masogange

Huyu alijipatia bahati ya kufahamika kwa kasi baada ya msanii belle 9 kumtumia kwenye nyimbo yake ya masogange ambayo Agnes alicheza kama Masogange, hadi Leo anafahamika kwa jina la masogange, ni kati ya watu wanaozungumzwa sana mitandaoni. Kesi yake ya madawa ya kulevya ilimuweka kwenye ulimwengu wa mastaa.

2. Romy Jones

Huyu jamaa ni ndugu wa Diamond. Amefahamika sana baada ya kuwa karibu na mwanamuziki Huyo, japokuwa ana maringo na nyodo kuzidi Diamond. Na yeye huyu sio mwanamuziki wala mcheza filamu.

3.Penny

Huyu bidada ni mtangazaji wa Dtv. Alikuwa hafahamiki apo awali, Jina lake lilivuma sana na kujikuta akiingia kwenye ulimwengu wa mastaa baada ya kujihusisha kimapenzi na msanii Diamond, ni miongoni mwa watu wanaofuatiliwa sana na kuzungumzwa.

4.Mange kimambi

Huyu alipata umaarufu kupitia mastaa kadhaa wa Tasnia mbali mbali apa bongo, alianza kuzinguana kwenye blogs na msanii wa maigizo Sintah, Ray( kuhusu kifo cha Kanumba), Shigongo na wengine kadhaa, wengi walitaka kumjua ni mtu wa aina gani baada ya kuanzisha bifu na mastaa wa bongo, hatimaye akajikuta akiogelea umaarufu.

5.Chaga Barbie

Huyu alijipatia umaarufu baada ya kujihusisha kimapenzi na msanii wa Kenya Prezzo, jina lake lilivuma zaidi pale walipozinguana na Prezoo hadi kufikia hatua ya kutoleana maneno mbofu mbofu mitandaoni. Ni kati ya watu wanaofuatiliwa sana mitandaoni.

6.Petit man wakuache

Huyu jamaa amefahamika kupitia Wema Sepetu, jina lake limevuma na kutajwa tajwa sana baada ya kuwa karibu na madame. Sio muigizaji wala mwanamuziki.

7.Najma

Huyu ni ex wa Mr blue, nae alianza kufahamika baada ya kujiingiza kwenye mahusiano na msanii huyo. Scandal yake ya kutoka na Diamond ilimuongezea credit kwa kiasi flan na kumfanya aongelew sana mitandaon, alishawah kujarib mziki pia na filamu.

8.Clement
Picha yake haijapatikana mpaka leo
 huyu alifahamika baada ya kujiingiza kwenye mahusiano na super star Wema Sepetu, ni kati ya watu wanaozungumzwa sana mitandaoni hadi kesho, japokuwa sura yake haifahamiki kihivyo, bado watu wanapenda kujua kuhusu yeye na maisha yake.

9.Ostadh Juma

Watu mjini wanatafuta umaarufu kwa kasi, baada ya kuzipata pesa kwa wingi , aliamua Ku manage wasanii kama PNC, dogo Janja na wengine japokuwa hana management skills nzuri. Kumrudisha dogo Janja dar es salaam na kumweka kwenye kundi lake la watanashati entertainment pamoja na kumpiga picha PNC alipokuwa akijaribu kumuomba msamaha kumemfanya aongelewe zaidi na kufuatiliwa maisha yake mbaya zaidi hadi ya wazazi wake kitu ambacho kimem cost kwa kiasi Fulani.

10. Kajala Masanja


Kwenye mtandao wa instagram ana followers karibia elfu thelathini na kitu, wote wametokana na promo ya maana kwa shoga yake Wema Sepetu, kutolewa rumande na Wema Sepetu kumemuongezea umaarufu zaidi na kuwa miongoni mwa watu wanaozungumzwa sana, jina la kajala limekaa sana mdomoni mwa Wema Sepetu, hivyo kumfanya apate mashabiki wengi zaidi kupitia Wema. Ni mcheza filamu za 
kibongo.
MANAIKI SANGA THE DON
Huyu jamaa amekuwa maarufu sana nchini na nje ya nchi baada ya kupiga picha na wanawake zaidi ya 400 zikiwa za utupu lakini baadae mastaa kibao kama Wema Sepetu, Irene Uwoya, Jackline Wolper na wengine walianza kupiga nae picha licha ya kukumbwa na kashfa hiyo.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king