Friday, January 22, 2016

NJAACHUPUCHUPU KUUA MPWAPWA: WANANCHI WASHINDIA MBOGA ZA MAJINI KUNUSURU MAISHA YAO, WAMTOLEA UVIVU MBUNGE WAO MWENYE TABIA YA KUKAA KIMYA BUNGENI, WAMTAKA ASIONE AIBU AOMBE MSAADA ILI KUOKOA MAISHA YAO, PICHA HIZI HAPA....!



WANANCHI WA MPWAPWA KIJIJI CHA MAKUTUPA KAMA WALIVYOKUTWA NA CAMERA ZA MASKANIBONGOTZ WAKIANDAA MBOGA ILI WACHEMSHE WAPATE KULA AMBAPO HALI YA JAA IMEKUWA TISHIO KUTOKANA NA MWAKA JANA MVUA KUSHINFWA KUNYESHA, AMBAPO WANANCHI HAO WAMEMTAKA MBUNGE WAO MHESHIMIWA GEORG LUBELEJE KUACHA KUKAA KIMYA BUNGENI AZUNGUMZE UKWELI KUHUSU HALI YA NJAA JIMBONI KWAKE ILI WAPATE MSAADA
 MHE: GEORG LUBELEJE  AMEOMBWA KUACHA TABIA YA KUKAA KIMYA BUNGENI BADALA YAKE APAZE SAUTI NA KUELEZA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOLIKABIRI JIMBO LAKE IKIWEMO NJAA NA UMASKINI ULIOKITHIRI HUKU WANANCHI WENGI WAKIHITAJI MSAADA KWENYE JIMBO LAKE HILO LA MPWAPWA
WAKAZI WENGINE WA KIJIJI CHA  MBORI KATA YA MATOMONDO WAKIPEMBUA MBEGU ZA MABOGA ILI WAFANYE CHAKULA.

 Na Mwandishi wa maskani bongo gazeti Mpwapwa. Wananchi wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma wamemjia juu mbunge wao mwenye tabia ya kukaa kimya awapo mjengoni na kumwambia asione aibu kusema ukweli kwamba anahitaji msaada wa hali na mali wa chakula ili awanusuru na kifo. 
Gazeti la Maskani Bongo ambalo lipo Wilaya humo kujonea na hali halisi ya njaa huku watu wengi wakionekana kuhitaji msaada wa hali na mali mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Mabwemazeru aliyejitambulisha kwa jina la Jemsi Luhunga alisema" Ndugu mwandishi kwanza tunawashukuru Maskani Bongo kufika huku kijijini na kujionea balaa la njaa kiukweli hali sio nzuri Serikali isipofanya jitihada za haraka tunaweza kuzungumza mengine"Alisema 
Nae Mama mmoja mjane toka kijiji cha Lupeta Chang'ombe aliyejitambulisha kwa jina la Mama Emy  alisema" Jamani chonde chonde tunaomba msisitieni Mbunge wengu Lubeleje asikae kimya bungeni kama miaka yote aweke wazi balaa hili la njaa ili Serikali itusaidie tunakufa jamani, asituchukulie sisi kama Mazombi kwa vile tayari yeye tumeshampa kula na familia yake tunachotaka atusaidie kuondoa balaa hili la njaa" Alisema 
Gazeti hilili lifanya jitihada za kumtafuta Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa ili azungumze jitihada wanazochukua ili kuondoa balaa hilo lakini kwa bahati mbaya hakuwepo ofisini na kudaiwa kuwepo Dodoma mjini.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king