Thursday, October 22, 2015

SIRI YA WASANII WA KIKE BONGO MOVIE KUJIUZA ZAFICHUKA : VICTORIA LUOGA AWACHANA LIVE..!

 Victoria Luoga msanii anaechipukia kwenye kiwanda cha Bongo Movie amewapa ushauri wa bure mastaa wa bongo movie hasa wale wanaojiuza



Na Anna Mdemu

Msanii chipukizi ambae pia ni mjasiriamali Victoria Luoga ametoa funzo kubwa kwa wasanii wenzake wanaokimbilia ustaa wakati hawana kitu hali inayopelekea mwisho wa siku wanajiingaza  kwenye ukahaba kutokana na njaa kali.
Victoria ambae ametamba vilivyo kwenye filamu ya Kivuri change na yeye amecheza kama Staa alisema” Ni ukweli Dada wasanii wengi wa kike wanakimbilia kuwa mastaa wakati hawana kitu au hawafanyi kazi nyingine zaidi ya  sanaa hali inayowapa shida wakati wanapokuwa na majina tayari ili hali hawana kitu hali inayopelekea kujitoa muhanga kwenye umalaya ili amradi wapate pesa za kujikimu” Alisema Luoga
Msanii huyo ambae ameanza kujitegemea tangu akiwa mdogo kwa kutafuta hela ambapo hadi sasa tayari ana vitega uchumi vyake ambapo sasa sanaa anafanya kwa kwa vile ipo kwenye damu na si vinginevyo hivyo hata kama sanaa ikizungua poa tu alisema msichana huyo.

Victoria kwa  sasa anamiliki Grocery kadhaa hapa mjini, pamoja na nyumba za kulala wageni licha ya umri wake kuwa mdogo lakini amefanya mambo makubwa  na mwisho aliwashauri wasanii wenzake hasa wanawake  wajitahidi kuwa na kitu kingine cha kufanya tofauti na sanaa ili iwasaidie kujikimu badala ya kutegemea sanaa tu ambayo kwa haraka haraka hailipi.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king