Mkuu wa kitengo cha Oparesheni ya kupambana na uharifu Kinondoni Swai Jakob Swai akiwa kazini
Waharifu
mbalimbali waliokamatwa wakiwa chini ya ulinzi mkali, pongezi kubwa kwa
Swai ya kujitoa kwa ajiri ya kuwasaidia wananchi.Swai Jakob Swai akiwa mbele ya Kito cha Polisi Oysterbay Polisi hivi karibuni.
Na Livingstone Mkoi
Wakazi wa Kinondoni meneo tofauti tofauti wamejitokeza na kumpongeza Askari shupavu mwenye nyota mbili aliyefahamika kwa jina la Swai Jakobu kwa kazi nzuri anayoifanya ya kupambana na uhairifu wa vibaka pamoja na uharifu mwingine kiasi cha kuwafanya kwa sasa wananishi kwa amani. Wakiongea na gazeti hili watu hao walisema" Jamani kiukweli ni lazima tushukuru huyu Afande Swai amekuwa msaada mkubwa sana kwetu hizi patro anazozifanya mara kwa mara zimekuwa msaada mkubwa sana kwetu" Alisema mmoja wa wakazi wa Kinondoni Mkwajuni aliyefahamika kwa jina la Mama Zai ambae ana miliki Salooni Aidha wananchi wengine waliongeza kusema kuwa Afande huyo ambae ni kipenzi cha watu ila ni adui wa mkubwa wa waharifu " Huyu Afande anaijua kazi yake vizuri na huwa hataki masihara awapo kazini ndiyo maana unaona hata vibaka wengi wameamua kuacha kuiba au kuvuta unga kwani huyo jamaa akikukamata hana msalie mtume ni moja kwa moja mahakamani kisha jela, hivyo uadilifu wake umesaidia sana kuondoa uharifu kwa kweli" Alisema Mwita ambae ni askari Jeshi Mstaafu mkazi wa Msasani
0 comments:
Post a Comment