Yasmeen Yakubu ambae ni mtalaka wa mwanamuziki nyota nchini Hammer Q.
Mwanamitindo mahali nchini Yasmeen Yakubu.
Yasmeen
Yakubu amemjibu mke wa aliyekuwa mumewe wa zamani Hammer Q, Salha
Abdala kuwa aache kumtafuta mchawi anaeivuruga ndoa yake badala yake
aangalie ndo yake kwani ndoa sio kama kuimba taarabu bali ni kazi ngumu
sana.
Mwimbaji
wa kundi la Dar M Taarab Salha Abdala akiwa na bandeji kichwani baada
ya kujeruhiwa vibaya na mumewe Hammer Q hivi karibuni katika ugomvi
ambao mwimbaji huyo alisema ulisabaisha na mtalaka mwenzake Yasmeen
Yakubu
Hammer Q.
Na Livingstone Mko
Mtalaka wa mwanamuziki nyota wa taarabu nchini Hammer Q aitwae Yasmeen
Yakubu ameibuka na kumpa onyo kali mke wa sasa wa mumewe huyo wa
zamani na kusema aache kumtafuta mchawi wa ndoa yake kwani ndo sio kama
kuimba taarabu bali inahitaji kutulia.
Akiongea
ndani ya ofisini za maskanibongotz hivi karibuni Yasmeen alisema hayo baada
ya mke huyo wa Hammer Q ambae pia ni muimbaji wa kundi la Dar modern
Taarab kumtuhumua kuwa yeye ndiye chanzo kupigwa nusra ya kutolewa
nafasi na mumewe.
Yasmeen
aliendelea kuieleza maskanibongotz alikuwa wiki iliyopita alikuwa nje ya
nchi alisikia taarifa toka kwa watu wake wa karibu kuwa Salha alikuwa
nahojiwa na kituo kimoja cha radio ndipo aliomtuhumua mke mwenza huo
kuwa ana mahusiano na mumewe.
Mwanamitindi
huyo alisema kuwa alishtushwa sana na taarifa hizo kwani yeye tangu
ameachana na Hammer miaka mitano iliyopita hajawahi kukutananae kwa
njia yoyote ile" Hivyo jamani namshauri tena huyo mwanamke akae chini
ili kujua tatizo anakosea wapi ili ajirekebishe ili asipigwe tena na
sio kukurupuka na kuanza kupakazia watu, mimi naishi na mchumbaangu na
familia yangu hivyo sielewi tuhuma anazonipakazia huyo mwanamke
zinatoka wapi" Alimaliza kusema Yasmeen
Credit: Maskanibongotz
0 comments:
Post a Comment