Tuesday, July 21, 2015

WAFAHAMU MASTAA WA NIGERIA WALIOCHUKUA MAAMUZI MAGUMU 2015, WA TANZANIA WATAKIWA KUWA MFANO..!


 
BOFYA HAPA KUONA FILAMU YA MSANII MANAIKI SANGA IITWAYO WAKE UP ILIYOWASHIRIKISHA WASANII ZAIDI YA 30 PAMOJA NA INATARAJIA KUTOKA MWEZI WA NNE
 
JAPOKUWA mwaka huu wa 2015 umepita nusu yake ni mengi yametokea katika ulimwengu wa burudani ambapo waburudishaji  wengi walioanza mwaka wakiwa ‘wapweke’ hivi sasa wana wenza wao waliofunga nao ndoa na wanategemea kufanya hivyo kabla mwaka huu haujaisha.
Mtandao wa Nigeriafilms.com umekuwa ukiweka kumbukumbu na sasa unaweza kuonyesha ndoa za ‘nguvu’ ambazo zimetamba katika nusu ya kwanza ya mwaka 2015. 
Paul Okoye na Anita Isama .
Ndoa ya kimila iliwakutanisha Peter, mmoja wa mapacha wa kundi la muziki la Psquare alipomchukua mpenzi wake wa siku nyingi na mama wa mtoto wake, , Anita Isama. Tukio hilo lilifanyika mwezi Januari huko Ikoyi, Nigeria.
Peter Okoye na Lola Omotayo-Okoye.
Kama ilivyokuwa kwa kaka yake, mwanamuzaiki  maarufu,  Peter Okoye, na mama wa watoto wake wawili, Lola Omotayo, waliimarisha uhusiano wao kwa kufunga ndoa huko Ikoyi.


Chris Attoh na  Damilola Adegbite.
Wawili hawa walioana siku ya Wapendanao ya Valentine -- Februari 14 – katika ndoa ya kimyakimpya jijini Accra, Ghana ambapo biharusi Damilola Adegbite alikutana na mpenzi wake, mtoto wa mfalme wa kikabila huko Ghana, Chris Attoh, kwenye mahojiano ya kipindi cha televisheni cha Mnet cha Tinsel.
Japokuwa wawili hao wanasema watafunga ndoa nchini Nigeria,  marafiki zao wanasema wana hamu ya kuona hilo linatokea kabla ya kumalizika kwa mwaka 2015.

IK Ogbonna na  Sonia Morales.
Mwigizaji maarufu wa filamu wa ‘Nollywood’, Nigeria, Ik Ogbonna na mpenzi wake Sonia Morales,  walifunga ndoa Jumatatu ya Juni, 29 2015 huko Serbia, Columbia; nyumbani kwa bi harusi.   Ndoa yao ilikuja siku chache baada ya wapenzi hao kupata mtoto wao wa kwanza Jumamosi ya Juni 20, 2015 ambaye walimpa jina la Ace.


Gbenro Ajibade na  Osas Ighodaro.
NI dhahiri Gbenro Ajibade bado ana furaha isiyomithilika kwa kumuoa kipenzi chake, Osas Ighodaro, ambaye hadi sasa bado wako kwenye fungate.  Wawili hao walioana Jumamosi ya Julai 4, 2015 jijini New York Marekani.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king