Wednesday, July 29, 2015

NAIBU SPIKA MH NDUGAI APIGA MTU NUSU YA KUMUUA KISA KURA ,JIMBONI KWAKE HALI TETE WANANCHI HAWATAKI HATA KUMUONA KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU ALIYOYAAHIDI, CHADEMA WAJIPANGA KUCHUKUA JIMBO KIURAINI KAMA CCM INAMRUDISHA TENA KUGOMBE UBUNGE...!

 
BOFYA HAPA KUONA  DEMO YA FILAMU YA MSANII MANAIKI SANGA IITWAYO WAKE UP ALIYOWASHIRIKISHA WASANII ZAIDI YA 30.

 Aliyekuwa Naibu Sika wa Bunge la Jamhuru ya Muungano wa Tanzania na aliyekuwa Mbunge wa  Kongwa Mh Job Ndugai  yuko kwenye hali mbaya jimboni kwake kutokana na wananchi wengi kumchoka hali inayomfanya kwa sasa kusaka kura kwa nguvu za kuomba kuoteuliwa hadi kufikia hatua ya kumpiga mgombea mwenzake hadi kuzila
Na Ripota wa Sadikitv
Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amejichimbia kaburi la kisiasa Jimboni kwake baada ya kumshambulia Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph Elieza Chilongani kwa gongo katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM
Hayo yametokea jana mnamo saa saa 10 jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini Kongwa.

Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe na ukorofi ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea nalo huku wasimamizi wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye kampeni.
Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye ngatunga) Alisimama kuuza sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini...
Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi..
Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu.
Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia "Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani."
Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa fimbo hiyo. aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..
Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa kichapo Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na kukimbia Eneo la Tukio..Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr. Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo huyo mgombea mwengine kiasi hadi watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio hilo ovu mkutano ulivurugika.
Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu walimbeba akiwa amezimia na kumkimbiz hospital baada ya kupata PF 3 toka polisi.
Hadi sadickTV Inaondoka hospitalini Dr alikuwa bado hajazinduka na madaktari walikuwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha ya mgombea huyo.
Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa tukio hilo lilirekodiwa na pengine ushahidi huo utatumika katika kumuengua Ndugai katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge kwa ticket ya CCM hasa baada ya watia wengine kuweka pingamizi mara mbili lakini bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia macho.
Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa kama haki itatendeka Ndugai atakuwa amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia KIAMA CHAKE RASMI KATIKA SIASA ZA JIMBO LA KONGWA kutokana na wananchi wengi kumkataa mbunge huyo kutokana na kushindwa kuwafanyia chochote cha maana zaidi ya kuineemesha familia yake kwa kuwapeleka shule za gharama, Pia mbunge huyo inadaiwa ameshindwa hata kusaidia watoto wasiojiweza kwa kuwafungulia hata mfuko maalum wa kuwasaidia.
‪#‎sadickTV‬ tunakuahidi kukuletea video ya tukio hili muda si mrefu

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king