MFUNGAJI bora wa kihistoria Afrika Kusini na mshindi wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Benni McCarthy (pichani kushoto) alivamiwa na watu wenye bastola Jumanne akiwa ananyoa nywele mjini Johannesburg, amesema wakala wake.
Watu
watatu wenye bunduki walivamia saluni ya Melrose alipokuwa ananyoa
nyota huyo mwenye umri wa miaka 37 mjini Johannesburg, na kupora pete ya
ndoa ya mkewe, saa na vitu vingine vya thamani. Hakujeruhiwa.
Wakala
wa McCarthy, Percy Adams alisema waporaji hao walimlenga mshambuliaji
huyo tu aliyeiwezesha Porto ya Ureno kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa
mwaka 2004 chini ya kocha Jose Mourinho katika saluni hiyo.
Waporaji
waliwapuuza watu wengine tisa waliokuwa kwenye saluni hiyo.
“Hawakumgusa mtu mwingine, hawakutaka fedha, hakuna walichotaka kutoka
kwake, walichukua walichokipata kwake na kuondoka,” amesema Adams.
McCarthy
ndiye mfungaji bora wa kihistoria wa Afrika Kusini kwa mabao yake 31,
yakiwemo nane katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1998
nchini Burkina Faso, ambako Bafana Bafana walishika nafasi ya pili.
Amecheza Ulaya, ikiwemo Ureno, Hispania na England katika klabu za Blackburn na West Ham.
Kwa sasa anasomea leseni ya ukocha ya UEFA katika klabyu ya Hibernian ya Scotland.
Browse » Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment