Thursday, May 28, 2015

HII KALI: WEMA SEPETU NA MAMAAKE WAZUSHA TIMBWILI ZITO BANDARINI WEMA AMCHAPA KOFI POLISI WASWEKWA LUPANGO MASAA 6. MASKANIBONGOTZ INAKUPA ISHU NZIMA..!


Na Mwandishi Wetu
Katika hali isiyokuwa ya kawaida staa wa bongo movie Wema Sepetu na Mamaake Miriam Sepetu hivi karibuni walizusha balaa kubwa bandarini huku Wema akidaiwa kumzaba kibao Polisi baada ya kuwazuia kupita sehemu ya VIP. maskanibongtz imetonywa
Habari za uhakika zilizonaswa na paparazi wa maskanibongotz zilisema kuwa Wema na Mamaake walifika kwenye bandarini hapo bila kufahamika walipokuwa wanakwenda na baada ya kufika hapo moja kwa moja Wema na Mamaake ambao wote walikuwa wamevaa miwani mieusi na waliingia kwenye geti la watu wanaosafiri kwenda Zanzibar na kwingineko na moja kwa moja waliingia kwenye sehemu ya VIP.
Lakini hata hivyo katika hali ya kushangaza Wema na mzazi wake walipita getini na kumchunia Askari aliyekuwepo bila hata kumsalimia hali iliyomfanya afande huyo kuwaita wawili hao ili kurudi kwake lakini Wema akiwa ameshikana mkono na mamaake hawakutii amri hiyo bila shuruti na walimpuuza afande huyo ambae baada aliwafata na kuwazuia ndipo afande huyo alipoishia kula kibao cha haja hadi kushika shavu lake kwa uchungu.
Hata hivyo Afande huyo aliamua kukumbushia mazoezi aliyopita Moshi ambapo alichachamaa na kuawarukisha kichurachura wawili hao kisha kuwasweka lupango sehemu moja iliyopo humo humo bandarilini.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho hakina hata chembe ya shaka kilisema Mama Wema alikuwa anatia huruma kwa mazoezi hayo na kumuomba Afande huyo awahurumie lakini haikusaidia kwani Afande huyo ambae inadaiwa anatoke Mkoa wa Mara alikuwa amepandisha mzuka.
Hata hivyo ilidaiwa Wema na Mamaake walikaa kwa masaa 6 ndani toka  saa nane mchana hadi kumi na mbili jioni, mtandao huu wa maskanibongotz ilifanya jitihada za kumtafuta Wema kupitia simu yake ya kiganjani ili kuzungumza nae staa huyo na kuweka bayana madai hayo lakini kwa bahati mbaya simu hiyo haikupatikana licha kupigwa kwa masaa 3.
Credit: maskanibongotz

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king