Staa wa filamu ya Wake Up Manaiki Sangu akiwa mbele ya mastaa mbalimbali walishiriki filamu hiyo ambayo imefananishwa na ile ya Expendables ya nje kwa kusheheni mastaa zaidi ya 30 huku wakiwa wamechuana vikali.
Kazi kazi wasanii Hemed Suleiman na Irene Uwoya wakiwa kwenye hisia kali wakati wakiigiza filamu hiyo ya Wake Up ya msanii Manaiki Sanga " The Don"
Mzee Majuto ambae amekuwa kivutio kikubwa ndani ya filamu hiyo ya Wake Up
Na Mwandishi Wetu
Msanii wa Bongo Movie na Bongo Flava nchini Manaiki Sanga amefanya kitu ambacho hakikuwahi kufanyika nchini toka 15 iliyopita tangu sanaa ya filamu ilipoanza baada ya kuandaa filamu iliyowakutanisha wasanii zaidi ya 30 ndani ya filamu moja.
Akiongea na gazeti hili muongzaji filamu hiyo Leah Richard
Mwendamseke “Lamata” Alisema kuwa filamu hiyo ambayo maandalizi yake yamemaliza
miezi sita hadi kukamilika kuigizwa kwake huku akimpa wakati mgumu sana na kuwa
historia kwake tangu aanze kuongoza filamu za nchini Tanzania.
Lamata aliwataja mastaa walioshiriki filamu hiyo iliyopewa
jina la “Wake Up” Irene Uwoya, Jackline Wolper, Gabo, Othuman Amri “King Majuto” Kajala, Yusuph
Mlela, Tausi, Aisha Boko, Hemed Suleiman, Quickrocker, Kupa,Duma, Mama Abdul,
Flora Mvungi, kwa upande wa wanaumziki ni Country Boy, Nas B akiwemo mwenyewe
Manaiki Sanga ambae ndiye staa wa filamu hiyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji wa msanii Manaiki Sanga
Bwana Livingstone Mkoi alisema kuwa filamu hiyo kwa sasa ipo kwenye hatua za
mwisho “ Tuko hatua za mwisho kumalizia na tayari tumepewa ofa kibao za kuiuza
filamu hiyo iliyosheheni mastaa hao na kampuni mbalimbali za usambazaji filamu zimeanza kupanda dau la kusambaza filamu hiyo ya kwanza nchini Tanzania kwa kuchezwa na mastaa wengi huku ikifananishwa na ile ya Expendables ya nje ya nchi" Alisema Mr Mkoi
0 comments:
Post a Comment