Wasanii
mbalimbali wanaunda kundi la Bongo Movie nchini ambao wameshiriki kwenye filamu
ya msanii Manaiki Sanga iitwayo Wake Up wamemtetea msanii mwenzao kuhusu kashfa
ya picha za uchi alizowahi kupiga miaka ya nyuma.
Wakiongea
na gazeti hili hivi karibuni wakati wakiigiza filamu hiyo iliyowashirikisha
zaidi ya wasanii 36 walisema kuwa binadamu wote wanatakiwa kusahau madhambi ya
mtu kwa vile yalishapita ni vyema watu wakaangalia ya sasa na yajayo.
Wasanii
hao ambao ambao kila mmoja aliongea jinsi anavyoona lakini kila mmoja
alionekana kumtetea Manaiki kwa tukio alilowahi kulifanya.
Mmoja
wasanii hao ambae nae ni mshiriki ni Jackline Wolper baada ya kuulizwa na
mwandishi wetu anazungumzia matukio ya ukatili ya msanii huyo kwa wanawake
aliyowahi kuafanya ambapo alijisema “ Kiukweli Manaiki aliwahi kuteleza kama
ambavyo angeweza kuteleza binadamu mwingine au mimi na wewe hivyo ni vyema tuka
sahau hayo tusiendelee kumuhukumu Manaiki kwa madhambi yaliyopita si vizuri”
Alisema Wolper
Aidha nae
Irene Uwoya ambae aliwahi kutuhumiwa kutembea na Manaiki yeye alisema hivi “
Ndugu yangu mimi upande wangu naweza kusema kuwa jamii inapaswa kumsamehe
Manaiki sisi sote ni binadamu na tunakosea ni vyema tukasahau yaliyopita tayari
picha ziko mitandaoni na kama anavyoeleza mwenyewe alipoteza Computer
yake na kulikuwa na picha zake za sili” Alisema Uwoya
Mzee
Majuto ambae ni swahiba mkubwa wa Manaiki alisema “Mwanangu binadamu
hatujakamilika Manaiki si kijana mbaya ndiyo maaa unaona wasanii wote hawa tunampa
sapoti amekuwa na ushirikiana na wenzake sana, kuhusu hizo picha ni jambo la
kusahau kwa vile lilishapita tugange yajayo watanzania subirini kuipokea filamu
yake mpya inaitwayo Wake Up ambayo ni kama zawadi kwa watanzania” Alisema
msanii huyo mkongwe
Kajala
Masanja ambae kwa sasa wameingia mkataba na Manaiki kwa ajili ya kufanya kazi
pamoja yeye upande wake alisema “ Ni kweli kati ya watu walioumia sana kuona
zile picha ni mimi Manaiki ni kama mdogo wangu ndiyo maana nimeamua kumchukua
na kuwa nae pamoja na kumuweka sawa kisaikolojia kwa vile tayari zile picha
zilikuwa zimemuathiri “ Alisema Kajala
Wasanii
karibia wote walioshiriki filamu hiyo yaExpendables ya Tanzania iitwayo Wake Up
iliwashirikisha wasanii zaidi ya thelathini na sita huku iliongozwa na Lamata
na kushutiwa na kampuni ya Manaiki Production iliyopo Itumbi Hotel.
Wasanii
walioshiriki filamu hiyo ya Wake Up ni Irene Uwoya, Jackline Wolper,
Gabo, Othuman Amri “King Majuto” Kajala, Yusuph Mlela, Tausi, Aisha Boko, Hemed
Suleiman, Quickrocker, Kupa,Duma, Mama Abdul, Flora Mvungi, Tracy Moshi,
Hemed Kavu “HK” kwa upande wa wanaumziki ni Country Boy, Nas B,
Kiss, Juta B, akiwemo mwenyewe Manaiki Sanga ambae ndiye staa wa
filamu hiyo na wengine wengi.
0 comments:
Post a Comment