Inaweza kuwa good news nyingine kwa mashabiki wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara Azam FC mwaka huu wa 2014 ambao sasa hivi wanatarajia kumsajili na kumshusha bongo beki wa Ivory Coast Pascal Serge Wawa toka klabu ya El Mereikh ya nchini Sudan.
Wawa ambaye ana umri wa miaka 28 ni beki ambaye amewahi kuichezea timu ya taifa ya Ivory Coast kwa wachezaji wenye umri chini miaka 23 ambapo alishiriki michuano ya kimataifa kwa vijana inayofanyika kila mwaka nchini Ufaransa ( Toulon) na pia amewahi kufanya majaribio kwenye timu ya ligi kuu ya Ufaransa ya Lorient.

Kabla ya kusajiliwa na El Mereikh mwaka 2010 Wawa alikuwa akiichezea timu ya Asec Mimosas ambayo aliichezea kwa muda wa miaka 7 tangu mwaka 2003.
Aliwahi pia kuja Tanzania akiwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast kilichoshiriki michuano ya Cecafa Challenge Cup na kufika fainali ambako walifunga wenyeji Kilimanjaro Stars 1-0 na alichezea kikosi hicho akiwa na mapacha walioko Azam FC leo hii ambao ni Tchetche Kipre na Bolou Kipre.
Wawa anatarajiwa kusaini kuichezea Azam Fc katika dili ambalo halijawekwa wazi thamani yake wala urefu wa mkataba.
0 comments:
Post a Comment