Thursday, October 30, 2014

USTADH ALIYENASWA KWENYE KIGODORO USIKU WA MANANE APIGWA MARUFUKU MSIKITINI. YADAIWA ALIKUWA MTU MUHIMU KWENYE NYUMBA HIYO YA IBADA...!

Na Sakina Shabani
Mzee mmoja ambae ni Ustadhi aliyefahamika kwa jina la Abuu Ramadhani "54" mkazi wa Mburahati Jijini Dar amepigwa marufuku kukanyaga kwenye nyumba ya ibada baada ya kunaswa akiwa kwenye kigodoro usiku mnene na mijimama iliyopinda.
Kwa mjibu wa mtu chanzo chetu kiliitonya Maskanibongotz kuwa mzee huyo alikuwa tegemeo kwenye msikiti ambao hakuutaja jina lakini upo maeneo ya Manzese lakini baada ya kunaswa kwa picha hiyo mzee huyo hatakiwi tena kugusa ardhi ya msikiti huo kwani tayari ameshakikuka utaratibu wa imani hiyo sani na yenye nidham Duniani.
Hata hivyo habari zaidi zilisema kuwa siku ya tukio mzee huyo alitoroka nyumbani kwake na kuicha familia yake kisha kwenda kwenye laana hiyo ya kigodoro, na ilielezwa kuwa mzee huyo ambae ni mwenyeji wa Mkoa wa Tanga amekuwa na mzuka na vigodoro hata vikipigwa mahara popote ili amradi asikie sauti hata kama alikuwa anakula chakula ataacha na kujichanganya.
CREDIT: MASKANIBONGOTZ

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king