Thursday, October 16, 2014

MISS TANZANIA KUPOKWA TAJI KWA KUDHALILISHA MASHINDANO HAYO. ATAPEWA MSHINDI NO 2. ALIDANGANYA VIBA ETI KAMA ALIANZA DARASA LA KWANZA AKIWA NA MIAKA 2. HATA HIVYO TUHUMA ZA RUSHWA YA NGONO ZAHUSIHWA...!



Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akionesha cheti mara baada ya kuhitimu masomo.


Mshtuko! Siku chache baada ya kutwaa Taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu ameibua mshangao wa aina yake kutokana na utata wa umri wake, Ijumaa limesheheni data.

Utata huo uliibuka saa chache mara baada ya shindano hilo kufanyika Oktoba 10, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo wadau mbalimbali walianza kuhoji.
UTATA WENYEWE HUU HAPA
Mara baada ya mrembo kutangazwa mshindi, habari za chini kwa chini zilidai kwamba Sitti alijinasibu kuwa ana umri wa miaka 18 na elimu ya (digrii mbili) (masters), mambo ambayo yaliwashtua wengi na kuanza kuhoji uhalali wa umri huo ukilinganisha na kiwango chake cha elimu.
“Mh! Haiwezekani, kama ana miaka kumi na nane atakuwa alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili?” Alihoji mdau mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini.
Hata hivyo kuna uwezekana wa kupokwa taji hilo kama kweli waandaji watataka kulinda heshima ya mashindano hayo. Na wadau mbalimbali wamesema huenda rushwa ya ngono ilitumika ili kuchakachua matoke.
CREDIT: MASKANIBONGOTZ

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king