Thursday, October 30, 2014

MH: KOMBA ATAKIWA KUACHANA NA URAFIKI NA VIBINTI VIDOGO NA KUTULIA NA FAMILIA YAKE, KWANI KUNA LENGO LA KUMMALIZA KISIASA.!

Na Sakina Shabani
Mashabiki na wanachama wa CCM Kata ya Hananasif Kinondoni Jijini Dar wamemshauri Mh Kaptein Komba Mbunge wa Mbinga Magharibi kuacha urafiki na vibinti vidogo kwa vile kuna mpango wa kumdhalilisha msimu huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.
Maskanibongotz ambayo ilinasa mazungumzo ya vijana CCM waliokuwa kwenye mchakato wa kura za maoni za kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa walisikika wakisema" Jamani waheshimiwa wetu hasa viongozi wa CCM msimu huu wa kuelekea uchanguzi Mkuu wanatakiwa kuwa makini kwa vile hali ya kisiasa kwa sasa sio nzuri wamepanga kuchafuliana"Walisema 
Hata hivyo wanaccm hao moja kwa moja akili zao walizielekeza kwa Mh Komba mara kadhaa amekuwa akikumbana kashfa za namna hiyo kutokana na huruma yake kwa vijana kwa kuwa nao karibu hususani mabinti, ambapo hivi karibuni Mh huyo alichafuka baada ya picha zake mbaya akiwa na kigori kimahaba lakini hata hivyo Mh huyo alikana na kusema picha hizo ni za kutengenezwa.
CREDIT: MASKANIBONGOTZ

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king