Wakati ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume huwarubuni wanafunzi wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za kielimu kwa kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako mwanafunzi wa kidato cha pili amemzalisha mwalimu wake.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 17 amemzalisha mwalimu wake mwenye umri wa miaka 25 katika shule ya sekondary ya umma ya Nkasi iliyopo katika mwambao wa ziwa Tanganyiaka.
Wanafunzi katika shule hiyo wamekuwa wakiendelea kumpongeza mwanafunzi mwenzao kwa kufanikiwakiwa kupata mtoto katika umri mdogo huku mzazi mwenzie akiwa na uhakika wa maisha kutokana na kuwa mwajiriwa wa serikali.
Imeeelezwa kuwa licha ya tukio hilo, mwalimu huyo aliyezaa na mwanafunzi wake bado anaendelea na kazi shuleni hapo huku darasani kukiwa na mzazi mwenzie. Akizungumza na mwandishi wa haabari hizi mjini Namanyere hivi karibuni mkuu wa sekondary ya Nkasi ndugu Amiamie Nanga alisema, Mwalimu huyo aliyezalishwa na mwanafunzi ameanza kazi shuleni hapo ikiwa ni mara yake ya kwanza kufundisha tangu atoke chuoni.
"Yameshatokea lakini haileti picha nzuri sana, lakini mimi nina uzoefu mkubwa sana na wakazi wa ukanda wa pwani wa ziwa Tanganyika kwao sio ajabu kabisa kuwa na uhusiano na mtu aliye kuzidi umri, iwe kwa mtoto wa kike au wa kiume wote ni sawa tu...
CREDIT: MASKANIBONGOTZ
Browse » Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment