Habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa Bongo ni kitendo cha mtangazaji mwenye jina kubwa wa Kipindi cha Maskani cha Redio Times FM, Gardner G Habash ‘Kepteini’ kutaka mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘
Jide’ ndiye aeleze ukweli juu ya ndoa yao.Akizungumza kwenye Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani kupitia Televisheni ya EATV chini ya ‘hosti’ wake, Salama Jabir, Jumanne iliyopita, Gardner alikataa kuzungumzia ndoa yake inayodaiwa kuvunjika.
Pamoja na mambo mengine ambayo aliyajibu kwa ufasaha, Gardner alipoulizwa juu ya habari zinazozungumzwa mtaani kuhusu kuvunjika uhusiano wake na Jide au Lady Jaydee, aligoma kulizungumzia kwa kigezo kwamba kipindi hicho kilimhusu yeye tu.




0 comments:
Post a Comment