Friday, May 30, 2014

Picha ya mwanamke aliyepiga magoti hospitali kubembeleza apatiwe dawa ya maumivu kabla ya kifo chake.


mwanamke
Unaweza kudhani matukio haya hutokea katika hospitali za kawaida tu. Hii ni ya kusikitisha zaidi, Picha hii ya mwisho inamuonyesha mwanamke mmoja aliyekuwa amezidiwa hospitali na akashindwa kupatiwa dawa hadi kuamua kupiga magoti akibembeleza apatiwe dawa ya maumivu tu kutokana na kuzidiwa kwake lakini wauguzi hawakumsaidia chochote hadi umauti ulimkuta.
mwanamke2
Siku mbili baada ya kutelekezwa na maafisa wa hospitali, mwanamama huyo Margaret Lamberty alipoteza maisha baada ugonjwa wake unaotibika kumzidi kutokana na kushindwa kupatiwa msaada.
Margaret alifikishwa hospitali ya chuo kikuu cha A&E Kaskazini mwa Staffordshire na wanafamilia yake akiwa na maumivu makali ya tumbo, Mtoto wake kike aitwaye Laura amesema kuwa baada ya kufika hospitalini hapo wauguzi walikuwa wakimuangalia tu bila kumpa msaada wowote ndipo mama yake akaamua hadi kupiga magoti akiwaomba wampatie dawa ya maumivu lakini hakusikilizwa na mtu.
mwanamke3
Baada ya kifo cha mwanamke huyo, Familia inapanga kuishtaki hospitali hiyo kwa kushindwa kutimiza wajibu wao hadi kusababisha kifo cha ndugu yao.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king