Wednesday, May 28, 2014

MABASI YA MWENDO KASI YA SHABIBY YATIA HOFU NCHINI, MENEJA WAKE ATEMA CHECHE MKOANI DODOMA ANGALIA KAURI YA MHESHIMIWA MWENYEWE..!

 Haya ni mabasi mapya ya Mh Shabiby yaliyoshushwa hivi karibuni
Na Livingstone Mkoi
Ujio wa mabasi mapya ya mwendo kasi ya Shabiby Line yamezusha balaa kubwa Mkoani Singida na Dodoma kwa wafanyabishara wengine kiasi cha kuwatia hofu ya kusitisha biashara hiyo waliokuwa wapinzani wake.
Habari toka Singida na Dodoma zinasema kuwa tangu mabasi mapya ya Shabiby yapatayo 26 yatue nchini na kufanya safari zake kati ya Dar, Dodoma na Moshi sasa safari mpya zimeanzishwa za Singida Dar na Moshi  lakini tayari mabasi mapya 8 yapo njiani kwa ajili ya luti hiyo mpya.
Hata hivyo kwa mujibu wa meneja wa kampuni hiyo ya Shabiby Saidi Shabiby ambae ni mdogo wa Mheshimiwa Shabiby alisema kuwa kuanzishwa kwa luti hiyo ni baada ya wanachi wa Singida kuiomba kampuni hiyo kufanya hivyo ili kuwasaidia kutokana ubovu wa mabsi mengine ambayo hayafai kupanda abiria.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king