Tuesday, October 13, 2015

ANGALIA TUKIO LA MTOTO MCHANGA ALIYEONESHA MAAJABU KWA LOWASA HUKO DODOMA, ATAJA JINA LA MGOMBEA HUYO MARA SABA KWA SIKU, WAZAZI WACHANGANYIKIWA WASEMA URAIS WA LOWASA NI MPANGO WA MUNGU. MASKANIBONGOTZ INAKUPA A-Z


 


MTOTO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GENIUS BOSS NGASA AMBAE NI MTOTO WA MWANDISHI WA HABARI NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA BOSS NGASA MEDIA INAYOMILIKI NA BLOG YA BOSS NGASA NA RADIO MPYA YA NGASA FM AMBAYO ITAZINDULIWA JANUARY MWAKANI AMEONSHA  MAAJABU MAKUBWA KWA KUTAJA JINA LA MGOMBEA URAIS WA UKAWA  EDWAD LOWASA TANGU AKIWA NA SIKU TATU TOKA AMEZALIWA.



  Mwandishi wa Habari Boss Ngasa akiwa na mwanae Genius.

 

Na Mwandishi wa Maskanibongotz-Dodoma

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mji wa Dodoma na vitongoji vyake vimekubwa na mshtuko kufuatia mtoto mdogo mwenye umri wa miezi minne kuongea na kutaja jina la Mgombea Urais kupitia Chama Cha Maendelea "CHADEMA" Bwa Edwad Lowasa hali iliyozusha mjadara mkubwa ndani ya familia hiyo na kuzusha taflani.

Habari za uhakika toka ndani ya familia ya Mwandishi huyo wa habari na mmiliki wa blog ya Bossngasa zilisema mtoto huyo alianza kuonesha maajabu hayo tangu akiwa na siku tatu toka amezaliwa " Ilikuwa usiku wakati familia hiyo ikiwa imelala na mtoto huyo ghafra walisikia sauti nyembamba ilikuwa ikitoka kwenye kinywa cha mtoto huyo iliyokuwa ikimtaja Lowasa Lowasa" Kilisema chanzo hicho

Hata hivyo baada ya kusikika kwa sauti hiyo wazazi wa mtoto huyo  waliogopa sana na hawakuamini kilichokuwa kinasikika toka kwa mtoto wao  lakini walimshkuru Mungu kwa utukufu huo licha ya kwamba hawakujua maana ya tukio hilo la kushangaza.

Aidha katika sauti hiyo pia kuna sauti nyingne ilikuwa ikisikika kwa mbali sana ambayo ilikuwa inasikika kwa shida kutokana na kuwa ndogo lakini kama ilikuwa inasema Rais Rais ukiacha hii ya Lowasa ambayo ilikuwa inasikika sana.

Baada ya mtandao huu wa maskanibongotz kupata habari hizo ulifanya mawasiliano na mwanahabari huyo maarufu Mkoani Dodoma ambae mwanae  huyo amezaa na mtoto wa kigogo "Jina linahifadhiwa" ambae pia dada huyo ni maarufu sana nchini, na alipatikana kupitia simu yake ya kiganjani na kueleza haya.

Na haya ndiyo majibu yake "Ndugu yangu hizo habari naweza kusema ni za kweli isipokuwa sikupenda ziwe ishu sanaaa, kutokana na mimi baba kubanwa na maadili yangu ya kazi ambayo yananizuia kuegemea chama kimoja ila ni kweli huyu mtoto katushangaza sana kutaja jina la Lowasa kuwa Rais" Alisema Boss Ngasa

Hata hivyo baba wa mtoto huyo aliongeza kusema kuwa yeye mwana habari ambae hana chama kila chama ni chake CHADEMA, CCM na vyama vingine vyote vina muhusu hivyo suala la mwanae anaomba lisichukue sura mpya na kumfanya aonekane yeye yupo CHADEMA hayo ni mtoto tu kama Mungu amemonesha hivyo kama Lowasa ni Rais basi ngoja tuone itakavyokuwa.

Credit; Maskanibongotz

 

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king