Sunday, August 7, 2016

RC MAKONDA, MSTAHIKI MEYA NA MKUU WA WILAYA KINONDONI WAZUSHA HOFU JIJINI DAR, WANANCHI WATAKA JUHUDI ZA HARAKA KUCHUKULIWA ILI KUNUSURI HALI HIYO....!

 Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar RC PAUL MAKONDA ambae amekiwa kivutio kwa wakazi wa Jiji hasa wanyonge kutokana na kujitoa muhanga kwenye mambo mbalimbali kwa ajiri ya kuwatete.
Utendaji wake mzuri toka akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndiyo uliopelekea Mheshimiwa Rais kumteua kuwa mkuu wa Mkoa. Ambapo Makonda ambaye amekuwa akifanya mambo yake kwa kwa haki na uwazi amesababisha amani kupatikani kwenye eneo lililokuwa hatari kwa usalama la mtaa wa NYAKASANGWE WAZO.
 Ambapo awali hapakuwa na kiongozi wa Serikali aliyeweza kuingia bila kuwa na gari sita za polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi, lakini cha kushangaza Makonda ambaye ni kama amemaliza mgogoro huo hadi sasa wananchi wanaendelea na majukumu yao huku watoto wakiendelea na elimu waliyokuwa wameikosa. 
Huku wakazi hao wakisubiri kupewa hati ya maeneo hayo ili wawe mawiliki halali, huku Makondo ambae toka akiwa mkuu wa Wilaya aliapa hatoruhusu kuvunjwa nyumba ya mtu yeyote kama walivyofanya viongozi waliopita na kupeleka wananchi kuichukia Serikali yao.
 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa WILLIAM LUKUVI amekuwa mmoja wa viongozi wanaofanya kazi kwa haki na usawa ambapo hali hiyo imepelekea wananchi wengi kurudisha imani kwa Serikali yao kwani mwanzo waliichukia kutokana na watu wachache walioshirikiana na mafisadi wa ardhi kuwaonea wananchi kwenye mtaa wa Nyakasangwe Wazo Jijini Dar ulioongozwa na Mwenyekiti wake Mchungaji Peter Bilebela.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe.Ally Hapi ambae anasubiriwa kwa hamu na wananchi hao mtaa wa Nyakasangwe na Kazaroho huku wengi wakitarajia kufanya mapokezi ya kihistoria, kwani pia ni mara ya kwanza kwa Mkuu huyo wa Wilaya tangu ateuliwe hivyo ni imani yao kuwa atakuja kumaliza mchezo kwa ushirikiano wa
Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob.

 Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob hivi karibuni alipokewa na maelfu ya wakazi wa Nyakasangwe alipofika katika eneo hilo kwa mara ya kwanza na kuahidi Manispaa imeshakaa na watu wanaojiita wenye mashamba na kuzungumza ili wamalize mgogoro huo hivyo siku hiyo alikuja kwa ajiri ya kupata maelezo ya upande wa wananchi na uongozi wa Serikali ya Mtaa.

Wananchi wengi wamepongeza mshikamo huu wa viongozi wa mji wa Dar na kusema wanatakaiwa kufanya kazi hivyo  wasijigawe kwani wataendelea kuwaumiza wananchi wanaowategemea kutokana na mji wa Dar kwa sasa kuongozwa na viongozi tofauti wa CCM na Upinzani hivyo umoja wao ndiyo utakaopelekea kufanikisha mengi waweke Siasa pembeni badala yake wajenge nchi.
Wakazi wa Nyakasangwe waliokuwa na mgogoro wa ardhi kwa miaka mingi lakini kwa sasa wameendelea na majukumu yao baada ya Makonda kumaliza mgogoro huo kwa njia ya amani baada ya kukaa na pande zote na kukubaliana waumalize kila pande itapata haki yake.
Mtandao  huu wiki hii umetembelea katika eneo hilo na kukuta ujenzi ukiendelea kwa kasi huku wananchi hao wakisema wanasubri tu ahadi za waheshimiwa
Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob na RC Makonda ya kuwapatia hati wakazi hao ili wawe na uhakika wa ardhi zao na kutaka juhudi hizo za haraka zichukuliwa kumaliza mgogoro huo kama walivyoahidi.
Hivyo kutokana na kauri za viongozi hao zinaonesha  dhahiri wanania ya dhati ya kumaliza mgogoro huo hali hiyo inaendelea kuleta matumaini mapya kwa wananchi kuwaamini viongozi wao wote wa Serikali na Upinzani.

Hata hivyo mshikamano huo wa Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob, RC Makonda, Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Ally Hapi na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa WILLIAM LUKUVI umedaiwa kuzusha hofu kubwa kwa mafisaidi wa ardhi walisababisha vifo vya wananchi na kuwavunjia watu nyumba zao bila kibali halali cha mahakama, kwani huenda baada ya kumaliza zoezi hilo wakafunguliwa mashtaka ya kufanya uharibifu huo na kuuwa watu.
Credit: Maskanibongotz

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king