Thursday, April 7, 2016

MUNGU MKUBWA: SHOGA ALIYEOKOKA NA KUMPOKEA MUNGU AELEZA JINSI ALIVYOACHANISHA NDOA YA MTU KISHA KUOLEWA NA MUME HUYO, MASKANIBONGOTZ

 ANT ASU ENZI HIZO WAKATI BADO AKIJISHUGHURISHA NA USHOGA AKIWA KATIKA POZI  SIKU YA SENDO OFF YAKE ILIYOFANYIKA NYUMBANI KWAKE KWENYE KOTA ZA MAGOMENI KABLA HAJIZAVUNJWA.
 ANT ASU AKIWA KWENYE POZI
KIJANA AMBAE NI BAUNSA MAARUFU JIJINI DAR AMBAE ALIAMUA KUMUACHA MKEWE NA KUMUOA SHOGA HUYO PICHANI JUU.
Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Hakika Mungu ni mkubwa hivi ndivyo tunavyoweza kusema kwani  hizi taarifa ni vyema kuzisikia kwa mtu mwingine na si kwa mtoto wako.
Naamini familia ya kijana huyu ambae amekuwa akijishughurisha na ushoga kwa miaka mingi hadi kuolewa na kuishi na mwanaume kwa miaka 6 ndani.
Huyu ni kijana ni maarufu sana hapa mjini anaitwa Ant Asu ambae kwa sasa huenda akawa ameipa ahueni familia yake na watu wa karibu kufuatia kuokoka na kuachana na mambo ya kishoga.
Akiongea na maskanibongotz kijana huyo alisema" Namshukuru Mungu kwa kweli kwa sasa naendelea vizuri nimeachana na hiyo tabia kwa sasa sitamani na nina umia sana nikikumbuka nilivyoiba wanaume za watu na kuwapagawisha kwa kuwapatia mapenzi motomoto" Alisema
Kijana huyo anaendelea kuieleza maskanibongotz alisema" Niwaombe radhi wanawake za watu kwa kweli hasa wanaoishi magomeni kwani walikuwa hawapumui wakiniona, lakini kwa sasa nimeokoka na nimekuwa mtu mwema na nahitaji maombi zaidi ili niendelee kuwa na hofu ya mungu na pia naimba radhi familia yangu najua imeumia kwa muda mrefu ila nimeamia kwa Mungu hakuna lisilojulikana' Alisema
Credit; Maskanibongotz

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king