Monday, August 3, 2015

MAGUFULI KUCHUKUA FOMU YA URAIS LEO, MAELFU YA WAFUASI WA CHAMA HICHO WATASHUHUDIA TUKIO HILO LIVE, ULINZI MKALI WAIMARISHWA ..!


Magufuli kuchukua fomu ya Urais leo, Dk. Slaa na CHADEMA? Mgombea Urais ADC + UKAWA na Zanzibar je?

Magaeti ya Agosti 4 2015 yako mtaani na vichwa vyake vikubwa vya habari, nimefanya jitihada ya kukusogezea zile zote kubwakubwa zilizoweka vichwa vya habari magazetini leo…
Prof. Ibrahim Lipumba aachia ngazi mgogoro mzito watikisa chanzo Lowassa… Zanzibar imesema kamwe haitotambua umoja wa UKAWA na maamuzi ya kutambua umoja huo ni ya Tanzania Bara na sio yao… Dk. John Magufuli kuliteka jiji kwa kuchukua fomu ya Urais leo ataongozana na mgombea mwenza Samia Saluhu Hassan kwenye ofisi za NEC.
CHADEMA yamuweka pembeni Dk. Wilbroad Slaa, Chama hicho kimeamua kumpumzisha kwa muda Dk. Slaa baada ya kutoafikiana na maamuzi ya Chama kumkaribisha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa.
ADC yaanza mchakatowa kumpata mgombea Urais wa Uchaguzi wa mwaka huu wa 2015, leo ikiwa ni siku ya mwisho ya watu kujiandikisha idadi wapiga kura Mil 2.6 waandikishwa kupiga kura na BVR  jijini hii ni aslimia 94% kwa jiji la Dar.
Rushwa yamtia kichefuchefu Rais Jakaya Kikwete Tanga kwenye makosa ya barabarani na aiomba Baraza la Usalama kuthibiti vitendo hivi kwa kutumia vifaa vipya vya Kiteknolojia na Mwasisi wa TANU na badaae CCM Mzee Peter Kisumo afariki dunia jana saa moja usiku kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, kifo chake kimesababishwa na maradhi ya figo.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king