Thursday, March 30, 2017

SHEKH SHARIF KHAMIS AREJEA NA SIRI NZITO KWA WATANZANIA, ASEMA ATAKACHOWAFANYIA WATANZANIA MMH…!

0 comments

Nyerere Shekh Sharif Khamis


Na Mwanaidi Othuman- Pazia Jeusi Tanzania
Baada ya ziara ya Kenya kwa takriban miezi mitano  kijana mwenye karama ya ajabu Shekh Sharif Khamis sasa amerejea nchini huku akitoa uwito kwa watanzania kutumia nafasi hiyo kufika kwake kwa ajiri  kupokea uponyaji kupitia dua atakazowaombie watanzania.

Akiongea na mwandishi wetu juzi wakati katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Shekh Sharif Khamis aliongea live na mwandishi wetu na kusema “ Ilikuwa nikitoka Kenya niende moja kwa moja nchini Uganda lakini kutokana na watanzania wengi wamekuwa wakihitaji huduma yangu na nimekuwa nikiwasiliana nao katika mitandao ya kijamii” Alisema 

Shekh Sharif Khamis aliongeza kusema  watanzania watumie nafasi hiyo kufika nyumbani kwake  Magomeni Mapipa Mtaa wa Takadir no35  na moja kwa moja watakutana nae.

 Shekh Sharif Khamis  aliongeza kusema kuwa maisha ya sasa yamekuwa na mambo mengi mikosi ridhiki zimekuwa ngum na hata wanabahatika kupata  hazikai katika mikono yao. Huu ni wakat wakumuomba MUNGU huo ndiyo uwito wake kwa watanzania, hivyo kwa vile MUNGU ametoa vipaya kwa waja wake hasa watu kama Yeye hivyo anamsihi kila mtu bila kujari dini yake kabila lake utaifa wake wafike kwake kwa ajiri kuombewa kuondokana na mikosi hiyo.

Dua z Sharif Khamis zimekuwa msaada mkubwa kwa watu mbalimbali katika nchi za Angola, Kongo, Libya, Afrika Kusini, Misri, Uturuk, Kenya Uganda, Zambia, Oman nk ambako kote huko amekuwa akifanya mambo makubwa katika dua zake ambapo.

Ikumbukwe kijana huyu ambaye ameanza kufanyakazi ya kumtumika Allah tangu akiwa na mwezi mmoja hadi leo na tangu akiwa na umri huo yeye amekuwa akiwatumikia watu kiasi cha kumfanya ashindwe kwenda shule za kidunia. Lakini MUNGU amekuwa akimfunulia kufanya makubwa sana katika maisha yake na ametaja namba yake ya simu kuwa ni +255 717688792.

Wote mnakaribishwa, hata wale wenye magonjwa sugu hao ndiyo anaashughurika nao sana, wenye mapepo ya kichawi nk ni nafasi yao.

Atakuwa nchini kwa miezi miwili tu

Source: Pazia Jeusi-Tanzania

 
SOMA ZAIDI ...

Monday, March 13, 2017

WEMA SEPETU ACHAFUA HALI YA HEWA DODOMA, WAJUMBE WAKONGWE WA CCM WAPANGA KUMRUDISHA KIMAFIA, BONGO MOVIE YAPASUKA VIPANDE VIPANDE, MASHABIKI NJIA PANDA…!

0 comments



Na Pazia Jeusi. Tanzania
Msanii wa Bongo Movie anayedaiwa kuwa na  wafuasi wengi kuliko msanii yeyote Tanzania Wema Sepetu amechafua hali ya hewa Mkoani Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo baadhi ya wajumbe katika mkutano huo wameonesha kusikitishwa kukosekana kwa Wema Sepetu kwenye ziara ya wasanii walikwenda Dodoma.

Wasanii hao waliotambulishwa katika mkutano huo na  Humphrey Polepole katibu mwenezi wa ccm na baadae wasanii hao kupongezwa na Rais John Magufuli kama ni wasanii wazuri.

Mwandishi wetu wa Pazia Jeusi ambaye alijipenyeza katika  ziara ya wasanii hao alisema kuwa pengo la Wema lilijidhihilisha wazi kwani msanii huyo  ni kipenzi cha  wajumbe wengi wa CCM kutokana na mvuto mkubwa aliokuwa nao katika jamii.

Habari zaidi ziliendelea kusema kuwa wajumbe wengi walionekana kumzungumzia Wema  muda wote, huku wakisema kuna haja ya kufanya michakato kabla ya mwaka 2020 kumrudisha CCM Wema Sepetu.

Mwandishi aliendelea kusema “ Naweza kusema ukweli msema kweli mpenzi wa MUNGU kama ambavyo huwa anapenda kusema Rais wetu, Wema Sepetu amedhihisha kama ana nyota kali wajumbe wengi wa CCM wanampenda sana”. Alisema mwandishi wetu wa Pazia Jeusi

Wana Ccm hao walifika mbali na kusema wanafahamu chanzo cha Wema kuondoka CCM ni utofauti wa  kiongozi mmoja wa Mkoa lakini kwa vile wamegundua hilo watahakikisha wanamrejesha nyumbani kabla ya uchaguzi mkuu ujao, wanaamini aliamua kwenda CHADEMA kwa jazba tu za kiongozi huyo wa mkoa.

Kuhama kwa Wema Sepetu na kutua chama pinzani kumeivuruga Bongo Movie na kwa sasa kama imepasuka vipande vipande ambapo mamilioni ya wafuasi wa Wema ambao awali walikuwa chama alichokuwa hivyo wapo waliomufuata na wapo waliobaki.

Source: Pazia Jeusi-Tanzania

 


SOMA ZAIDI ...

Saturday, March 11, 2017

EXCLUSIVE NEWS: MSANII MANAIKI SANGA APOTEZA FAHAMU BAADA YA KULA HASARA YA MILIONI MIA TANO. NI YA POMBE KALI AINA YA VIROBA ZINAZOTAKIWA KUTEKETEZWA, ALAZWA HOSPITAL…!

0 comments


 Msanii Manaiki Sanga kulia akiwa na Stan Bakora
  Msanii Manaiki Sanga kulia akiwa Irene Uwoya nchini Nigeria walipokwenda kushuhudia utoaji tuzo mbalimbali za Filamu barani Africa.

Na Pazia Jeusi. Tanzania
Msanii wa Bongo Movie Manaiki Sanga mwanazoni mwa wiki hii ameadaiwa kuzimia ziaidi ya mara nne kutokana na hasara ya kupoteza mali zenye thamani ya milioni mia tano za aina ya vinywaji vikali Viroba.

Akiongea na Pazia Jeusi mdogo wa masanii huyo aliyjitambulisha kwa jina la Ayubu Sanga alithibitisha kutokea tukio hilo la kaka yake kunusurika kifo kwa presha hadi kupelkea kuzimia kutokana na kupotza mali hizo.
Ayubu alisema “ Ni kweli bro amepatwa na hali hiyo hadi sasa ameshatoka Hospital huku Mufindi nyumbani ambapo hadi sasa anaendelea vizuri lakini Daktar wetu amekaa asiongee na simu kwa zaidi ya wiki moja hivyo hii simu yake ninayo mimi na nipo nae mbali kwani hatakiwi kusikioa chochote” Alisema Ayubu

Msanii Manaiki ambaye pia ni mfanyabiashara alikuwa anamiliki maduka kadhaa ya viwanji Mkoani Iringa, Mbeya na Morogoro. Habari zaidi zilieleza kuwa msanii huyo ana maduka ya kuuza jumla na lejaleja vinywaji hivyo na wakati amri ya Waziri Mkuu ilipotolewa ya kupiga marufuku matumizi ya voroba na wafanyabiashara wote kupewa muda kumaliza mzogo wao yeye alikuwa nchini Afrika Kusuni.
Na aliporejea akakuta tayari muda waliokuwa wamepewa umeshaisha.
Source: Maskanibongotz

SOMA ZAIDI ...

MWANAMUZIKI MR BLUE APIMANA MISURI NA JESHI LA POLISI, ASHUKA NA NDEGE NCHNI KENYA AKITOKEA NJE AINGIA NCHINI KIMYA KIMYA, AISHI KAMA DIGI DIGI PAZIA JEUSI LINAKUPA A-Z...!

0 comments
 KAMANDA SIRRO VS RC MAKONDA
MWANAMUZIKI MR BLUE.

Na Mwandishi wa Pazia Jeusi- Tanzania
Mwanamuziki wa bongo flava  Herry Sameer aka Mr Blu ambaye hivi karibuni alitajwa kati ya  watu wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya  amerejaea nchini kimya kimya na sasa imeelezwa anaishi kama digidigi kukwepa mkono wa Serikali.
Habari za uhakika zilizothibishwa na matandao huu wa habari za uchunguzi wa Pazia Jeusi "Fichua" umegundua kuwa mwanamuziki huyo yupo nchini na alirejea hivi karibuni toka nchi za nje alikokuwa ameenda kwa kazi isiyojurikana.

Hata wakati Mkuu wa Mkoa anataja majina ya wanamuziki wanaodaiwa kujihusisha na madawa ya kulevya ile kwa kutumia ama kuuza na yeye jina lake lilitajwa  hivyo wakati wenzake wakiwekwa lupango yeye alikuwa nje ya nchi.

Pazia Jeusi "Fichua" ilipata taarifa za mwanamuziki huyo kurejea nchini kwa siri huku ukielezwa kuwa mwanamuziki huyo alishuka na ndege nchini Kenya kisha akapanda basi hadi kufika Dar kwa siri kubwa kwa kuogopa Polisi.

Hata hivyo cha kushangaza mwanamuziki hadi sasa hajaenda kuripoti kituo cha Polisi cha kati kama alivyotakiwa na Mkuu wa Mkoa licha ya habari zake kuvuja kama hivi kuwa yupo nchini hali inayoonesha kama  amelitunishia misuri Jeshi la Polisi.
Mtandao huu wa Pazia Jeusi uliwasiliana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum kutaka kujuwa kama mwanamuziki huyo alisharipoti kituoni kama alivtakiwa ama laa, ambapo simu ya Kamanda Sirro iliita bila mafanikio hadi habari hii inaruka hewani muda huu.
Herry Sameer aka Mr Blu imedaiwa kwa sasa amejificha katika Hotel ya Itumbi, nyumbani kwake hata ukienda humkuti.
Source: Pazia Jeusi-Tanzania 
SOMA ZAIDI ...

Thursday, March 9, 2017

HALI YA HATARI; RAIS MAGUFUL NA WAZIRI LUKUVI WANTED, JESHI LA POLISI LATAHADHARISHWA, WABAYA WATAKA KUTUMIA SAKATA LA MAKONDA KUFANYA UMAFIA…!

0 comments



Na Livingstone Mkoi- Maskanibongotz
 
Wananchi wa mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa wanaoishi kwenye mgogoro wa ardhi kwa zaidi ya miaka kumi na tano sasa wameingia hofu kuhusu hatma ya makazi yao dhidi ya mafisadi wa ardhi ambao tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda aingie kwenye sekeseke la tuhuma za vyeti batili.

Wakiongea na waandishi wetu wa mtandao wa Maskanibongotz wakazi hao wapatao elfu nne walisema  tangu ishu ya Makonda ilipozuka watu hao wanaodai wenye mashamba wamekuwa wakionekana karibu kila siku wakiwa na magari ya kifahari katika makazi yao jambo linalowapa hofu kubwa.

Hofu waliyonayo wakazi hao ambao hadi sasa wameshahakikiwa katika eneo hilo na kubakisha kupewa hati za Serikali tu ili wayamiliki kihalali makazi yao, wamesema wasi wasi huenda watu hao wenye mashamba ambao “ Mafisadi Ardhi” Wakatumia udhaifu wa matatizo ya Makonda kuwaonea mwanzo jinsi walivyobomolewa makazi yao bila kibali cha mahakama huku watu kumi na tatuu wakipoteza maisha.

RC Makonda ndiye aliyekuja kusambaratisha mtandao huo wa ufisaidi na kufanikiwa kuwaweka huru wakazi hao ambapo awari watu waliokuwa wameyaterekeza mashamba hayo zaidi ya miaka ishirini na kuacha msitu huku majambazi wakitumia maficho ya uharifu hadi Mkuu wa Mkoa miaka hiyo Yusuph Makamba alipoamuru Serikali ya mtaa kugawa eneo hilo.

Watu hao wenye mashamba walijaribu kutumia nguvu kubwa ya kifedha kuwaondoa  wananchi kwa kutumia Polisi, wenye sialaha, na mabomu, na mabaunsa kwa kuwabomolea hadi kupelekea wakina mama kujifungua kabla ya muda, huku wengine wakipoteza maisha, walifanyiwa ukatili huo bila msaada wowote katika utawala uliopita hadi alipokuja Makonda kurudisha amani.

Makonda alionekana adui mkubwa dhidi ya mafisadi hao kiasi cha kumchukia kwa kuwatetea wananchi hao wanyonge, katika neo hilo palikuwa hapaingiriki zaidi ya kuwindana na mishare ya sumu kwa wananchi na bunduki kwa Polisi, ilifika mahara wakazi hao walipewa kesi  kuwa wao sio raia wa Tanzania kwa lengo la kuwaondoka tu, lakini kipindi cha kupiga kura wananchi hao waliachwa kwa muda ili wapige kura baada ya kumalizika  kupiga kura waliisoma namba.

Baada ya maongezi na wananchi hao waandishi wetu walifika ofisi za Serikali ya mtaa wa Nyakasangwe zinazoongozwa na Mtumishi wa Mungu Peter Bilebela kwa ajiri ya kupata ukweli wa jambo hilo.

Mwenyekiti huyo alianza kuzungumzia jambo hilo “ Kwanza kabisa niwashukuru ndugu waandishi kwa kufika huku kwetu kujionea hali halisi, kuhusu hizi taarifa za kuonekana kwa watu hao ndani ya magar ya kifahari ninazo licha ya kwamba mimi sijafanikiwa kuwaona kwa macho yangu” Alisema

Kiongozi huyo aliongeza kusema” Kwa vile wananchi wangu ndiyo wapo huko mtaani naamini kabisa taarifa hizo ni za kweli kwani katika mitaa yetu tunaishi kwa ushirikiano mkubwa hivyo wanapoona kitu tofauti lazima watanifikishia taarifa hizo” Alisema
Hata hivyo mwenyekiti huyo aliongeza kusema kuwa wananchi wake kweli wapo kwenye hofu kubwa juu ya hatma ya Makonda ambaye kwao wanamchukulia kama shujaa kutokana na alichokifanya katika mitaa hiyo kwa kurudisha amani iliyokuwa imetoweka miaka mingi iliyopita.

Mwisho, Mwenyekiti huyo kwa niaba ya wananchi wake ambao wamekuwa wakimsumbua kila siku wakiwataka  viongozi wakuu wa nchi  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini, Mhe. William Lukuvi  siku moja wafike katika mtaa wao huo wa Nyakasangwe kata ya Wazo.  Kumaliza mgogoro huo ili wananchi waanze kulipa kodi za viwanja  na majengo kwani Serikali inapoteza mamilioni ya shilingi kwa kukosa kukusanya kadi kutokana na uchelewaji wa kuwapimia wananchi viwanja na kupewa hatimiliki.

Lakini pamoja na hayo wakazi hao wameomba  Jeshi la Polisi kuweka tahadhari juu ya  watu hao wenye mashamba kwani wakijaribu kufanya jambo kuleta uvunjifu wa amani hali inaweza kuwa mbaya kwani safari hii hawatokubari kuonewa kama walivyofanya kwa utawala wa Rais Kikwete na kusisitiza huu ni utawala wa Magufuli ambao hautaki uonevu na upo kwa ajiri ya wanyonge.
Source: Maskanibongotz
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini, Mhe. William Lukuvi
SOMA ZAIDI ...

Wednesday, December 14, 2016

NILIAHIDIWA USTAA KAMA NINGETOA RUSHWA YA NGONO KWA MR CHULZ- TRACY MOSHI…!

0 comments
Msanii Tracy Moshi ”Breen”

Mr. Chuz na Kabula aliyezaa nae mtoto mmoja.

Na Mwandishi Wetu
Msanii mchanga kwenye kiwanda cha filamu Tanzania Tracy Moshi ”Breen” ameibuka na kumwaga mboga jinsi msanii na Director Tuesday Kihangala 'Mr. Chuz' alivyomuaidi ustaa kama angetoa uroda.
Msanii huyo toka Mkoa wa Tanga ambaye ametambulishwa vyema kwenye filamu alizocheza kama filama ya msanii Manaiki Sanga Wake Up, Our Teacher,Behind The Pastor, Ngema na filamu ya kimataifa ya Going Bongo, alisema bila kuwa na msimamo na anachokifanya  'Mr. Chuz' alifanyia udharirishaji huo.
Akipiga stori na gazeti hili hivi karibuni msanii huyo alisema jinsi alivyoshawishiwa kwenda kufanya usahir wa wa moja ya filamu ya Mr. Chuz “ Kaka kwa mara ya kwanza nilipigiwa simu na Mzee Magari akaniambia Mr. Chuz anataufuta wasanii wa dizaini kama yangu hivyo kwa vile mimi nina vigezo nikasema poa ntakwenda huko Jijini Dar” Alisema Breen
Msanii huyo aliendelea kuongea kuwa kutokana nay eye kuwa msanii mwenye ndoto kubwa katika tasinia ya sanaa ya tz basi alifunga safari toka Tanga hadi Dar na moja kwa moja alikwenda Makondo Ccm ndiko zilipo ofisi za msanii huyo.
Baada ya kufika huko Makongo akiwa ameongozana na msanii mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Preshazi na mara baada ya kufika huko alikuta wasanii wengi huki akiitwa mmoja baada ya mwingine na ilipofika zamu yake ya kuingia kwa bosi huyo ndipo alipoanza kumleta mapicha picha.
Breen anasema “ Nilipoingia tu Mr. Chuz alianza kusema mimi ndiye staa wake mpya hivyo wala sihitahi usahiri nimepita moja kwa moja hivyo nitoke nje ila nisiondoke hadi amalize kuwafanyia usahiri sanii wengine” Alisema
Cha kushangaz msanii huyo anasema Mr. Chuz alipomaliza kazi alianza kumletea habari hizo za mapenzi huku akiweka wazi kabisa kama atatoa kiburudisha basi atamfanya kuwa taa wa katika filamu zake , huku akimpigia mfano msani Jini Kabula, na Jack ambao walikubari kutoa uroda lakini amewapa ustaa hadi leo umewasaidia.
Breena anasema alishindwa kukubaliana na matakwa ya Mr. Chuz na kuamua kuondoka lakini jambo hilo akaamua kumueleza Mzee Magari ambaye nae alisikitishwa sana na tukio la msanii huyo kwani tabia kama hizo zimekuwa zikiwakatisha tamaa wasanii wachanga. 
Hata hivyo msani huyo anasema ameamua kuliweka wazi jambo hili ili kuwanusuru wasanii wengi wachanga ambao wamekuwa wakitoa uroda kwa waongza filamu ili wawapatiea nafasi za kucheza filamu zao jambo ambalo sio sahihi.
Baada ya taarifa hizi gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Mr. Chulz kupitia no yake ya kiganjani ili ajibu tuhuma hizi na aeleze kama anamfahamu msanii Breen lakini simu yake iliita bila mafanikio hadi gazeti hili linakwenda mitamboni jana, lakini mtandao huu unaendelea kumsaka Chulz ili ajibu tuhuma hizo ambazo pia zimekuwa zikilalamikiwa sana na wasanii wachanga kwa  Madirectors wengine wanawataka kutoa tamu tamu ndipo wapewe nafasi za kucheza filamu.


Source Maskanibongotz

SOMA ZAIDI ...

Sunday, August 7, 2016

RC MAKONDA, MSTAHIKI MEYA NA MKUU WA WILAYA KINONDONI WAZUSHA HOFU JIJINI DAR, WANANCHI WATAKA JUHUDI ZA HARAKA KUCHUKULIWA ILI KUNUSURI HALI HIYO....!

0 comments
 Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar RC PAUL MAKONDA ambae amekiwa kivutio kwa wakazi wa Jiji hasa wanyonge kutokana na kujitoa muhanga kwenye mambo mbalimbali kwa ajiri ya kuwatete.
Utendaji wake mzuri toka akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndiyo uliopelekea Mheshimiwa Rais kumteua kuwa mkuu wa Mkoa. Ambapo Makonda ambaye amekuwa akifanya mambo yake kwa kwa haki na uwazi amesababisha amani kupatikani kwenye eneo lililokuwa hatari kwa usalama la mtaa wa NYAKASANGWE WAZO.
 Ambapo awali hapakuwa na kiongozi wa Serikali aliyeweza kuingia bila kuwa na gari sita za polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi, lakini cha kushangaza Makonda ambaye ni kama amemaliza mgogoro huo hadi sasa wananchi wanaendelea na majukumu yao huku watoto wakiendelea na elimu waliyokuwa wameikosa. 
Huku wakazi hao wakisubiri kupewa hati ya maeneo hayo ili wawe mawiliki halali, huku Makondo ambae toka akiwa mkuu wa Wilaya aliapa hatoruhusu kuvunjwa nyumba ya mtu yeyote kama walivyofanya viongozi waliopita na kupeleka wananchi kuichukia Serikali yao.
 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa WILLIAM LUKUVI amekuwa mmoja wa viongozi wanaofanya kazi kwa haki na usawa ambapo hali hiyo imepelekea wananchi wengi kurudisha imani kwa Serikali yao kwani mwanzo waliichukia kutokana na watu wachache walioshirikiana na mafisadi wa ardhi kuwaonea wananchi kwenye mtaa wa Nyakasangwe Wazo Jijini Dar ulioongozwa na Mwenyekiti wake Mchungaji Peter Bilebela.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe.Ally Hapi ambae anasubiriwa kwa hamu na wananchi hao mtaa wa Nyakasangwe na Kazaroho huku wengi wakitarajia kufanya mapokezi ya kihistoria, kwani pia ni mara ya kwanza kwa Mkuu huyo wa Wilaya tangu ateuliwe hivyo ni imani yao kuwa atakuja kumaliza mchezo kwa ushirikiano wa
Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob.

 Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob hivi karibuni alipokewa na maelfu ya wakazi wa Nyakasangwe alipofika katika eneo hilo kwa mara ya kwanza na kuahidi Manispaa imeshakaa na watu wanaojiita wenye mashamba na kuzungumza ili wamalize mgogoro huo hivyo siku hiyo alikuja kwa ajiri ya kupata maelezo ya upande wa wananchi na uongozi wa Serikali ya Mtaa.

Wananchi wengi wamepongeza mshikamo huu wa viongozi wa mji wa Dar na kusema wanatakaiwa kufanya kazi hivyo  wasijigawe kwani wataendelea kuwaumiza wananchi wanaowategemea kutokana na mji wa Dar kwa sasa kuongozwa na viongozi tofauti wa CCM na Upinzani hivyo umoja wao ndiyo utakaopelekea kufanikisha mengi waweke Siasa pembeni badala yake wajenge nchi.
Wakazi wa Nyakasangwe waliokuwa na mgogoro wa ardhi kwa miaka mingi lakini kwa sasa wameendelea na majukumu yao baada ya Makonda kumaliza mgogoro huo kwa njia ya amani baada ya kukaa na pande zote na kukubaliana waumalize kila pande itapata haki yake.
Mtandao  huu wiki hii umetembelea katika eneo hilo na kukuta ujenzi ukiendelea kwa kasi huku wananchi hao wakisema wanasubri tu ahadi za waheshimiwa
Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob na RC Makonda ya kuwapatia hati wakazi hao ili wawe na uhakika wa ardhi zao na kutaka juhudi hizo za haraka zichukuliwa kumaliza mgogoro huo kama walivyoahidi.
Hivyo kutokana na kauri za viongozi hao zinaonesha  dhahiri wanania ya dhati ya kumaliza mgogoro huo hali hiyo inaendelea kuleta matumaini mapya kwa wananchi kuwaamini viongozi wao wote wa Serikali na Upinzani.

Hata hivyo mshikamano huo wa Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob, RC Makonda, Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Ally Hapi na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa WILLIAM LUKUVI umedaiwa kuzusha hofu kubwa kwa mafisaidi wa ardhi walisababisha vifo vya wananchi na kuwavunjia watu nyumba zao bila kibali halali cha mahakama, kwani huenda baada ya kumaliza zoezi hilo wakafunguliwa mashtaka ya kufanya uharibifu huo na kuuwa watu.
Credit: Maskanibongotz

SOMA ZAIDI ...

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king